Serikali ya Tanzania imetangaza
kuzisimamisha kwa muda stesheni mbili za redio ,radio 5 na Magic FM kwa
madai ya kumtusi rais Magufuli na kuchochea ghasia nchini.
Waziri wa mawasiliano Nape Nnauye amesema ameagiza kamati ya maadili kuzichunguza idhaa hizo na kupendekeza hatua zaidi kuchukuliwa dhidi yake.
![]() |
Waziri wa Mawasiliano Nape Nnauye |
Kulingana na muungano wa upinzani nchini humo CHADEMA,mikutano hiyo kwa jina UKUTA ,inalenga kupinga kuidhinishwa kwa sheria ya uhalifu wa mitandaoni inayokandamiza uhuru wa kujieleza ,kufutwa kazi kwa wafanyikazi wa serikali kiholela pamoja na marufuku ya mikutano ya kisiasa ya upinzani.
Ubalozi wa Marekani mjini Dar es Salaam umetoa ushauri wa kusafiri kwa raia wake ukiwaonya kutozuru maeneo ambayo mikutano hiyo itafanyika.
No comments:
Post a Comment