Viongozi wa chama cha upinzani cha
Chadema Nchini Tanzania walioshikiliwa jana jioni na kuhojiwa na jeshi
la polisi na baadaye kuachwa kwa dhamana, wanatarajiwa kurudi tena kikuo
kikuu cha polisi leo kwa maojiano zaidi.
Edward Lowassa ni miongoni mwa watakaofika polisi kuhojiwa zaidi |
Kupanga mikakati ya kutekeleza kile wanachokiita Operasheni Ukuta.
Inayotarajiwa kufanyika septemba mosi ikilenga kupinga kile wanachokiita ni kubanwa kwa demokrasia kwa serikali ya awamu ya tano.
Polisi waliwashikilia viongozi hao kufuatia kukiuka amri iliyotolewa na jeshi la polisi mwishoni mwa juma lililopita kupiga marufuku mikutano yote ya ndani ya vyama vya siasa.
Kufuatia mauaji ya askari polisi wanne yaliyotokea nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Waliokamatwa ni mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, katibu mkuu Dk. Vicent Mashinji, naibu Katibu mkuu bara John Mnyika na makamu mwenyekiti Zanzibar Said Issa
No comments:
Post a Comment