Most Popular

Hakuna siri tena, Kenyatta asaini kuwa sheria muswada wa haki ya kupata taarifa



Muswada wa haki ya kupata taarifa nchini Kenya wa mwaka 2015, hatimaye umetiwa saini na Rais kuwa sheria, ukiruhusu raia wa Kenya kupata taarifa kwa uhuru kutoka Serikalini pamoja na ofisi nyingine za uma.

Muswada huu ni miongoni mwa miswada mingine 9 ambayo Rais Uhuru Kenyatta ametia saini kuwa sheria juma hili.

Rais Uhuru Kenyatta, akitia saini moja ya miswada kuwa sheria hivi karibuni, juma hili ametia saini muswada wa sheria ya kupata taarifa kuwa sheria rasmi.
Miswada mingine ni pamoja na ile ya mkaguzi wa hesabu za Serikali, muswada wa fedha za matumizi ya ziada, Muswada wa baraza la taifa la mitihani, muswada wa haki ya ardhi asilia, muswada wa haki za kueleza tamaduni, muswada wa utunzaji wa misitu, muswada wa sheria ya ardhi na ule wa biadhaa za kilimo.

Kipengele cha sheria ya haki ya kupata taarifa, kifungu namba 35 cha katiba ya Kenya, kinaipa mamlaka tume ya mahakama na bodi maalumu iliyoundwa kuhakikisha utekelezwaji wa sheria hiyo mpya.

Sheria hii mpya, sasa unaondoa ukiritimba uliokuwepo awali kutoka kwa taasisi fulani za Serikali ambazo zilikuwa zinasifika kwa kuwanyima wananchi taarifa kwa kile ofisi hizo zilikuwa zikidai ni za siri.

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Transparency, linasema sheria ya haki ya kupata taarifa ni suala la lazima kwa ofisi za uma kutoa taarifa kuhusu Serikali na taasisi zake, kuhusu inachofanya, wafanyakazi wake na muundo wa mishahara.

Sheria hii pia inalazimisha taasisi nyingine za Serikali kuelezea kwa uma hatua ambazo imechukua, sera au maamuzi kwa wananchi wake ikiwa watataka kufahamu.
Posted By: MJOMBA ZECODER

Hakuna siri tena, Kenyatta asaini kuwa sheria muswada wa haki ya kupata taarifa

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger