Most Popular

Mgombea wa upinzani Gabon adai kushinda uchaguzi wa rais

Jean Ping mgombea mkuu wa upinzani wa kiti cha urais huko Gabon alidai jana Jumapili kuwa, ameshinda uchaguzi licha ya kambi hasimu inayoongozwa na Omar Bongo nayo kutoa madai kama hayo.
Ping alisema jana kuwa amechaguliwa na kwamba anamsubiri Rais anayemaliza muda wake amuite na kumpongeza. Jean Ping ameyasema hayo siku mbili kabla ya kutangazwa matokeo rasmi ya uchaguzi wa rais.
BWANA PING
 Ping ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari na wafuasi wake huko Libreville mji mkuu wa Gabon. Mgombea huyo mkuu wa upinzani aliyechuana katika uchaguzi wa Jumamosi hii na Ali Bongo Rais wa hivi sasa wa Gabon amemtuhumu tena Ali Bongo kuwa alifanya udanganyifu hata hivyo akasema, njama hiyo ya kambi ya mahasimu imesambaratishwa.
Posted By: MJOMBA ZECODER

Mgombea wa upinzani Gabon adai kushinda uchaguzi wa rais

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger