Wakati huu nchi ya Gabon ikikabiliwa na machafuko
ya mara baada ya uchaguzi mkuu ulioshuhudia kurejea madarakani kwa Rais
Ali Bongo Ondimba, wataalamu wanasema kuwa udanganyifu wa chaguzi barani
Afrika unazidi kuwa mgumu, shukrani kwa mashirika ya kijamii ambayo
yamekuwa yakifuatilia chaguzi mbalimbali na kukosoa pamoja na kuenea kwa
teknolojia ya simu za mkononi.
Ijumaa ya wiki iliyopita,
kiongozi mkuu wa upinzani nchini Gabon, Jean Ping alijitangaza kuwa
mshindi na Rais halali wa Gabon na kutaka kurudiwa upya kwa uhesabuji wa
kura, kufuatia madai ya Rais Bongo kudai kuwa aliibuka mshindi kwa
zaidi ya kura elfu 6 katika uchaguzi wa Agosti 27 mwaka huu.![]() |
Waandamanaji raia wa Gabon wakiandamana jijini Paris, Ufaransa, September 3, 2016 |
Mathias Hounkpe, meneja wa taasisi ya siasa na utawala wa Afrika Magharibi OSIWA, anasema kuwa kadri miaka inavyozidi kwenda, udanganyifu kwenye uchaguzi unazidi kuwa mgumu kufanywa na viongozi walioko madarakani.
Uwepo wa waangalizi wa ndani na wale wa kimataifa, pamoja na uwepo wa tume huru zisizofungamana na upande wowote, vimechangia kwa sehemu kubwa kuruhusu kufanyika kwa chaguzi zilizokuwa huru na za haki na kuzuia wizi na udanganyifu wa kura au kubadilisha matokeo.
Aboubacry Mbodji, katibu muuu wa shirika la haki Afrika RADDHO katika nchi za Afrika
![]() |
Waandamani raia wa Gabon waandamana barani Ulaya. |
Mashirika ya kijamii, uwepo wa vyombo vya habari na urahisi wa wananchik kutumia teknolojia ya mawasiliano kusambaza taarifa, ni kichocheo tosha kilichofanya chaguzi nyingi sasa barani Afrika kufanyika kwa uhuru na uwazi.
No comments:
Post a Comment