Rais
Barack Obama wa Marekani na Rais Xi Jinping wa China wameendelea na
tofauti zao juu ya masuala ya kiusalama kuhusiana na shughuli za majini
za China katika Bahari ya China Kusini pamoja na mfumo wa ulinzi wa
kuzuia makombora wa Marekani huko Korea Kusini.
Viongozi hao wawili walijadiliana kwa takribani saa nne Jumamosi jioni katika mji wa Hangzhou nchini China. Viongozi hao wamekutana baada ya mataifa yao kuchukua hatua ya kuridhia mkataba wa Paris wa kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa inayoongeza joto duniani.
Viongozi hao wawili ambao mataifa yao yanaongoza duniani katika uzalishaji wa hewa ya ukaa walielezea kwamba uamuzi huo wa kuridhia ni hatua muhimu katika utekelezaji wa makubaliano ya mkataba wa Paris.
Kuhusiana na uendelezaji wa nyuklia na makombora unaofanywa na Korea Kaskazini, viongozi hao walikubaliana kuimarisha ushirikiano wao kuhakikisha kuwa hakutakuwa na nyuklia katika rasi ya Korea na pia kutekeleza kikamilifu maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Kuhusu shughuli za majini za China katika Bahari ya China Kusini, Rais Obama walimweleza Rais Xi wa China kwamba wakubaliane na hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi iliyotolewa na Julai mwaka huu.
Rais Xi alijibu kwa kusema kwamba China itatatua migogoro inayoihusu kwa njia ya amani kwa mazungumzo ya moja kwa moja na nchi zinazohusika. Aliitaka Marekani kutekeleza wajibu wake wa kuimarisha amani na usalama katika Bahari ya China Kusini.
Hata hivyo Rais Xi alipinga mpango wa Marekani wa kupeleka mfumo wa kuzuia makombora katika anga huko Korea Kusini. Aliitaka Marekani kuheshimu maslahi ya kimkakati na usalama ya China.
Kwa upande wake rais Obama wa Marekani alisisitiza kwamba nchi yake lazima ihakikishe usalama wa washirika wake.

No comments:
Post a Comment