Mahakama ya kijeshi ya Misri imetoa hukumu ya vifungo vya kuanzia miaka miwili hadi maisha jela kwa watu 418 ambao ni wanachama na wafuasi wa harakati ya Kiislamu ya Ikhwanul Muslimin.
Mahakama hiyo imetoa hukumu kwa watu 350 bila ya wenyewe kuwepo mahakamani za kuanzia miaka 25 hadi kifungo cha maisha jela. Washtakiwa 68 waliokuwepo mahakamani wamehukumiwa vifungo vya kati ya miaka miwili hadi kumi jela.
Washtakiwa hao wamekabiliwa na mashtaka ya kuwa wanachama wa 'kundi lililopigwa marufuku' na 'kuharibu mali za umma na taasisi za polisi'.
![]() |
Hukumu kali zikiwemo za vifo zimetolewa dhidi ya wafuasi wa Ikhwanul Muslimin |
Kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa mahakamani, mnamo mwezi Agosti 2013, watu hao walivamia kituo cha polisi cha al-Minya katikati mwa Misri na kupambana na askari polisi.
Imeelezwa kuwa watu hao walichukua hatua hiyo baada ya jeshi kutumia nguvu kuwatawanya wafuasi wa Ikhwanul Muslimin waliokuwa wamekusanyika katika maeneo mawili ya mji mkuu Cairo na kusababisha kuuawa mamia ya watu.
Itakumbukuwa kuwa mahakama ya Misri imemhukumu kifungo cha maisha jela kiongozi wa harakati ya Ikhwanul Muslimin Muhammad Badie pamoja na wanachama wengine 35 wa harakati hiyo.
![]() |
Muhammad Badie, kiongozi wa Ikhwanul Muslimin |
Tangu mwezi Julai 2013 baada ya jesh,i likiongozwa na Abdel Fattah el Sisi kumwondoa madarakani Muhammad Morsi, rais aliyechaguliwa kidemokrasia, utawala wa Misri umetumia mkono wa chuma kuikandamiza vikali harakati ya Ikhwanul Muslimin.
![]() |
Muhammad Morsi, amehukumiwa adhabu kadhaa ikiwemo ya kifo |
Kwa mujibu wa taasisi za kutetea haki za binadamu, tangu wakati huo hadi sasa, hatua kandamizi za serikali ya el Sisi zimesababisha watu zaidi ya 1,400 kuuawa, 22,000 kufungwa jela na mamia ya wengine kuhukumiwa kifo kwa makundi
No comments:
Post a Comment