Daraja la vioo lililojengwa juu nchini Uchina ililosifiwa kwa kuvunja rekodi lilipozinduliwa siku 13 tu zilizopita limefungwa.
![]() |
Lilipozinduliwa, maafisa waliendesha gari lililokua limejaa watu na kuvuka daraja kuthibitisha namna daraja lilivyo salama |
Lakini Kituo cha televisheni cha Marekani CNN kimesema kuwa msemaji amewaambia kuwa daaja hilo linaloelea juu "limekuwa likitembelewa na wageni wengi kupita uwezo wake ".
Amesema kuwa hakuna ajali iliyowahi kutokea na daraja halikuwa na ufa wala mpasuko wowote.
Daraja hilo lenye urefu wa mita 430, ambalo ujenzi wake uligarimu $3.4 milioni, linaunganisha mabonde mawili ya milima ya Zhangjiajie, katika jimbo la Hunan.
![]() |
Daraja lingine la vioo la kutisha liko katika mkoa Uchina wa Hunan |
Lilipofunguliwa lilisemekana kuwa daraja refu zaidi kwa kimo na upana zaidi lililotengenezwa kwa vioo duniani.
![]() |
Wageni wakitembea juu ya sakafu ya vioo kwenye daraja la Zhangjiajie lililopo kwenye mkoa wa kusini mwa Uchina wa Hunan Province Jumamosi, Agostu. 20, 2016 |
Akijibu kuhusu tangazo hilo, mmoja wa watumiaji wa mitandao ya kijamii aliandika : "Nimelipa kila kitu na sasa mnasema mnafunga...Mnanitania?
No comments:
Post a Comment