Japani na Marekani zimesaini makubaliano juu ya ushirikiano katika kuendeleza uzalishaji wa nishati ya joto ardhi barani Afrika.
Chini ya makubaliano hayo, serikali za nchi hizo mbili zitakuza uwekezaji kwenye vyanzo vya nishati vilivyo rafiki kwa mazingira barani humo. Nchi hizo mbili zitalenga katika maendeleo ya uzalishaji wa nishati ya joto ardhi katika eneo la Afrika Mashariki.
Ni asilimia 30 tu ya watu barani Afrika wanaotumia nishati ya umeme. Kuhakikisha upatikanaji wa vyanzo vipya vya nishati imekuwa ni suala linalohitajika haraka kutokana na uchumi wa eneo hilo kukua.
Kuelekea utiaji saini wa makubaliano hayo jana Alhamisi, Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japani-JICA pamoja na mashirika ya misaada ya Marekani, waliendesha kongamano jijini Nairobi nchini Kenya juu ya maendeleo ya nishati ya umeme.
Afisa wa JICA alisema kuwa baadhi ya maeneo barani Afrika yana mifumo ya kijiolojia inayofanya iwe rahisi kupata mvuke wenye kiwango cha juu cha joto kutoka ardhini. Afisa huyo alisema kuwa Japani inaweza kutumia teknolojia yake ya uzalishaji nishati ya joto ardhi iliyoiendeleza kutokana na kuwepo kwa volkano nyingi nchini humo.

No comments:
Post a Comment