Most Popular

Rekodi ya kasi ya mtandao wa 4G katika simu yavunjwa

Kampuni ya Finland Elisa inasema imefanikiwa kupata kasi ya Gigabait 1.9 kwa sekunde, ikisema hiyo ndio kasi ya juu zaidi kuwahi kupatikana.

Rekodi ya kasi ya mtandao wa 4G katika simu za rununu yavunjwa
Huduma hiyo ya simu yenye kasi zaidi inaweza kupakua Filamu ya Blu Ray kwa muda wa sekunde 44.

Lakini wachanganuzi wana wasiwasi kwamba kasi hiyo inaweza kutumika moja kwa moja katika mtandao halisi ulimwenguni.

Elisa imesema kuwa imetumia teknolojia iliotolewa na kampuni ya China ya Huawei kutoa kasi ya upakuzi katika mtandao wa simu uliokaribia kiwango cha 2Gbps .

Ukilinganisha kasi yake ya mtandao ni 300Mbps ambayo iko chini mara sita.
Mkurugenzi mkuu Veli -Matti Mattila amesema: Tunajua kwamba hakuna kasi kama hii iliotangazwa na mitandao mingine.
Posted By: MJOMBA ZECODER

Rekodi ya kasi ya mtandao wa 4G katika simu yavunjwa

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger