Msemaji wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran
amesema, Rais Hassan Rouhani ametoa amri ya kudhaminiwa fedha
zinazohitajika kwa ajili ya kujenga vinu viwili vipya vya nyuklia humu
nchini.
![]() |
Kinu cha nyuklia cha Arak, nchini Iran |
Kamalvandi ameongeza kuwa, wiki mbili
zilizopita, ujumbe wa Iran ulielekea nchini China na hivi sasa pande
hizo mbili ziko katika mazungumzo kuhusiana na kukifanyia ukarabati wa
kimsingi kinu cha nyuklia cha Arak humu nchini.
Msemaji wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki
ya Iran aidha amesema, miswada ya mikataba ya kukifanyia ukarabati wa
kimsingi kinu cha maji mazito ya nyuklia cha Arak imeshaandikwa.
Ameongeza kuwa, mikataba hiyo itakuwa na mambo mengi ya kila namna
ambayo yanahitajia vikao na mazungumzo mbalimbali kuyajadili.
Aidha amesema, Iran itashirikiana pia na
nchi za Ulaya katika miradi yake ya nyuklia, na ushirikiano huo utakuwa
zaidi upande wa kudhamini zana na vifaa vinavyohitajika kwa mujibu wa
hati rasmi katika nyuga tofauti.
No comments:
Post a Comment