Biashara baina ya nchi za Afrika yasaidia kukuza uchumi
Ripoti hiyo inasema, biashara kati ya nchi za Afrika bado ni ya chini ikilinganishwa na sehemu nyingine za dunia.
Biashara baina ya nchi za Afrika ni asilimia 16 ya jumla ya biashara kote barani humo katika mwaka wa 2014 huku bidhaa za viwandani zikichangia asilimia 60 ya biashara ya kikanda barani Afrika.
Mapato ya jumla ya ndani yaani (GDP) kwa miji mikubwa barani Afrika, ikiwa ni pamoja na Johannesburg, Cape Town, Lagos na Luanda, yanatarajiwa kuongezeka, kutokana na ukuaji na ubora wa miundombinu.
Akitoa maoni yake kuhusu ripoti hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa DHL Express katika kanda ya kusini mwa jangwa la Sahara Hennie Heymans alisema, kuna fursa nyingi za kuongeza biashara kati ya nchi za Afrika, hasa kwa kuzingatia manufaa ya makubaliano ya Biashara Huria kati ya jumuiya tatu za kikanda, EAC, SADC na ECOWAS.
Kwa mujibu wa Heymans, nchi ambazo zingetaka kukuza biashara baina yao ni muhimu kufikiria muda na gharama zinazohusiana na usafirishaji wa bidhaa.
Ansema biashara barani Afrika zinaendelea kupata shinikizo katika hali ya sasa ya kiuchumi na kukumbwa na ushindani wa ndani na wa kimataifa na wakati mwingine zinakosa uwezo wa kujenga minyororo imara ya ugavi.
Kwa mujibu wa Heymans, kufanya maamuzi ya kimkakati kuagizia huduma za ugavi kunaweza kuleta mchango muhimu kwa faida ya biashara.
Ikiwa ni bara lenye ukuaji wa kasi zaidi wa tabaka la kati duniani, Afrika ni soko kubwa lenye wateja wanaotafuta upatikanaji rahisi wa bidhaa za aina mbalimbali.
No comments:
Post a Comment