Serikali ya Saudi Arabia imeamua kuifunga shule yake ya pekee nchini
Ujerumani, baada ya kulalamikiwa kwa muda mrefu kwamba huenda ikawa
inatumika kupandikiza na kueneza siasa kali.
Ubalozi wa Ufalme wa Saudia mjini Berlin unasema skuli hiyo ifahamikayo kama King Fahd Academy iliyopo katika kiunga cha Bad Godesberg, karibu na mji mkuu wa zamani wa Ujerumani Magharibi, Bonn, itafungwa mwanzoni mwa mwaka ujao.
Taarifa iliyotolewa jana na ubalozi huo inasema uamuzi huo umechukuliwa kama sehemu ya juhudi za Saudi Arabia kutoa elimu bora kwa raia wake popote pale walipo, lakini kwa kuwa Ujerumani inafahamika kuwa moja ya nchi zinazotoa elimu bora kabisa duniani, sasa hapana tena haja ya kuwa na chuo chake ndani ya ardhi ya Ujerumani.
Mnamo mwaka 2003, mamlaka nchini Ujerumani ziliichunguza skuli hiyo
kuona ikiwa ina mafungamano na mtandao wa al-Qaida na makundi mengine ya
Kiislamu.
Tuhuma zimekuwa zikielezea kwamba skuli hiyo inaweza kutumika kusambaza itikadi za Kiislamu ndani ya taifa hili la magharibi, na tangu wakati huo mjadala umekuwa ukiendelea baina ya pande hizi mbili kusaka suluhisho la pamoja.
Kwa sasa, skuli hiyo ina wanafunzi wapatao 150 na walimu 30, ambao wanafuata mtaala wa Saudia, ingawa pia hufundisha masomo kwa viwango vya kimataifa katika Kidato cha Tatu na Nne.
Suala la sera mpya za Saudi Arabia
Saudia haifungi skuli hii pekee nchini Ujerumani. Ujenzi wa skuli yake nyengine kama hiyo uliokuwa ukiendelea katika mji mkuu, Berlin, nao pia unaripotiwa kusitishwa.
Hata hivyo, taarifa ya ubalozi wa Saudia juu ya kufungwa kwa skuli hii imekuja katika nyakati zisizotegemewa, hasa linapohusika suala la ushirikiano wa karibu kati ya mataifa ya Magharibi na taifa hilo la Ghuba kwenye kile kinachoitwa vita dhidi ya ugaidi.
Lakini mkurugenzi wa masuala ya Mashariki ya Kati katika Taasisi ya GIGA mjini Hamburg, Henner Fürtig, ameaimbia Deutsche Welle kwamba kufungwa kwa skuli hii kunahusiana moja kwa moja na mageuzi yanayoendelea nchini Saudi Arabia kwenyewe, ambako Mwana Mfalme Mohammed bin Salman, anashinikiza kufanyika marekebisho muundo wa Dira ya 2030 iliyotangazwa mapema mwaka huu.
Ndani ya mpango huo, kuna orodha kubwa ya makato kwa matumizi yasiyo ya
lazima na pia muundo wa serikali wenye ufanisi unaolenga kuifanya nchi
hiyo kutoendelea na utegemezi wake kwa mapato ya mafuta.
Kwa mujibu wa Fürtig wa Taasisi ya GIGA, kufungwa kwa skuli hii pia ni jaribio la Saudi Arabia kubadili taswira yake barani Ulaya, kwani "haiwezekani kuwa serikali mjini Jeddah haifahamu utata na tuhuma za siasa kali ambazo zinatajwa dhidi ya skuli yake hiyo."
Ubalozi wa Ufalme wa Saudia mjini Berlin unasema skuli hiyo ifahamikayo kama King Fahd Academy iliyopo katika kiunga cha Bad Godesberg, karibu na mji mkuu wa zamani wa Ujerumani Magharibi, Bonn, itafungwa mwanzoni mwa mwaka ujao.
Taarifa iliyotolewa jana na ubalozi huo inasema uamuzi huo umechukuliwa kama sehemu ya juhudi za Saudi Arabia kutoa elimu bora kwa raia wake popote pale walipo, lakini kwa kuwa Ujerumani inafahamika kuwa moja ya nchi zinazotoa elimu bora kabisa duniani, sasa hapana tena haja ya kuwa na chuo chake ndani ya ardhi ya Ujerumani.
Skuli ya King Fahd Academy mjini Bonn, Ujerumani, ambayo inamilikuwa na serikali ya Saudi Arabia itafungwa rasmi mwanzoni mwa mwaka 2017. |
Tuhuma zimekuwa zikielezea kwamba skuli hiyo inaweza kutumika kusambaza itikadi za Kiislamu ndani ya taifa hili la magharibi, na tangu wakati huo mjadala umekuwa ukiendelea baina ya pande hizi mbili kusaka suluhisho la pamoja.
Kwa sasa, skuli hiyo ina wanafunzi wapatao 150 na walimu 30, ambao wanafuata mtaala wa Saudia, ingawa pia hufundisha masomo kwa viwango vya kimataifa katika Kidato cha Tatu na Nne.
Suala la sera mpya za Saudi Arabia
Saudia haifungi skuli hii pekee nchini Ujerumani. Ujenzi wa skuli yake nyengine kama hiyo uliokuwa ukiendelea katika mji mkuu, Berlin, nao pia unaripotiwa kusitishwa.
Hata hivyo, taarifa ya ubalozi wa Saudia juu ya kufungwa kwa skuli hii imekuja katika nyakati zisizotegemewa, hasa linapohusika suala la ushirikiano wa karibu kati ya mataifa ya Magharibi na taifa hilo la Ghuba kwenye kile kinachoitwa vita dhidi ya ugaidi.
Lakini mkurugenzi wa masuala ya Mashariki ya Kati katika Taasisi ya GIGA mjini Hamburg, Henner Fürtig, ameaimbia Deutsche Welle kwamba kufungwa kwa skuli hii kunahusiana moja kwa moja na mageuzi yanayoendelea nchini Saudi Arabia kwenyewe, ambako Mwana Mfalme Mohammed bin Salman, anashinikiza kufanyika marekebisho muundo wa Dira ya 2030 iliyotangazwa mapema mwaka huu.
Mwana Mfalme Mohammed bin Salman anatajwa kupigania mageuzi ya kiuchumi ambayo yamechochea maamuzi ya kuifunga skuli ya Saudia nchini Ujerumani. |
Kwa mujibu wa Fürtig wa Taasisi ya GIGA, kufungwa kwa skuli hii pia ni jaribio la Saudi Arabia kubadili taswira yake barani Ulaya, kwani "haiwezekani kuwa serikali mjini Jeddah haifahamu utata na tuhuma za siasa kali ambazo zinatajwa dhidi ya skuli yake hiyo."
No comments:
Post a Comment