Uchunguzi umebaini kuwa, kirusi cha Zika 
kinahatarisha maisha ya watu zaidi ya bilioni mbili katika nchi kadhaa 
za mabara ya Afrika na Asia.
  | 
| Mtoto aliyeathirika na kirusi cha Zika | 
Kwa mujibu wa makala iliychapishwa Ijumaa katika jarida la 
kitiba la 'The Lancet Infectious Diseases' , watu wanaoishi katika nchi 
zenye watu wengi za Nigeria, India na Indonesia wanakabiliwa na hatari 
kubwa zaidi ya kukumbwa na ugonjwa huo hatari. Hii ni kwa sababu 
wasafiri 5,000 huwasili katika nchi hizo kila mwezi kutoka nchi ambazo 
zinakabiliwa na mkuripuko wa Zika.
Brazil ndiyo chimbuko la mbu wanaosambaza kirusi cha Zika ambacho 
sasa kimeenea katika nchi 46 duniani tokea kuibuka kwa mara ya kwanza 
mwaka 2015
Kirusi hicho pamoja na mambo mengine husababisha wanawake wajawazito 
kujifungua watoto wenye vichwa vidogo na walio na matatizo ya ubongo.
  | 
| Add caption | 
Watu zaidi ya milioni 1.5 nchini Brazil wameambukizwa kirusi hicho na
 Wizara ya Afya ya nchi hiyo imesema watoto wasiopungua 580 wamezaliwa 
na maradhi ya microcephaly yanaosababishwa na kirusi cha  Zika.
 
 
No comments:
Post a Comment