Mmwanamke huyu mtangazaji,
anayesadikika kuwa na umri wa miaka sabini hivi, amekuwa akipewa jukumu
la kutoa matangazo muhimu zaidi ya taifa Korea Kaskazini.
Ri Chun-hee amewahi kulia, akacheka na kusema kwa sauti katika runinga ya taifa ya Korea Kaskazini katika kipindi cha zaidi ya miaka arobaini aliyofanya kazi.
Leo, amekuwa tena kwenye runinga kutangaza kutekelezwa kwa jaribio la tano la bomu la nyuklia Korea Kaskazini.
Hakuna anayefahamu umri wake hasa, lakini anadhaniwa kuwa na miaka sabini hivi.
Haya hapa ni mambo tunayoyafahamu kumhusu:
Hupenda rangi ya waridi
Sana vazi lake la Kikorea la chima jeogori, a well-known Korean dress.Alilivaa akitangaza kutekelezwa ka jaribio la bomu la haidrojeni Januari mwaka huu.
Lakini hubadilisha wakati mwingine.
Alivalia mavazi meusi na kuonekana kutekwa na huzuni akitangaza vifo vya viongozi wa Korea Kaskazini.
Huaminiwa sana na watawala
Inaarifiwa kwamba Kim Jong-un humtaka yeye awasilishe binafsi ujumbe wa chama chake kwa ulimwengu.Ndiye aliyetangaza vifo vya viongozi wa awali: Kim Il-Sung na Kim Jong-Il.
Ri Chun-hee majuzi alitangaza kufanikiwa kwa Korea Kaskazini kurusha satelaiti ya kuzunguka dunia kwa kutumia roketi. Hilo lilishutumiwa kama njama ya kufanyia majaribio kombora la masafa marefu.
Hubadilisha hisia.
Anaweza kusema kwa sauti na hata kulia akitangaza.
Pia, huzungumza kama mtu mwenye mamlaka akifikisha ujumbe wa viongozi wa Korea Kaskazini.
Anaonekana kuwa maarufu sana.
Chun-hee huishi Pyongyang, na huonyeshwa runingani akiwa na watu wengi wanaomtazama, kupiga makofi na wakati mwingine kulia.
Majuzi alsema anataka kuacha kazi ya utangazaji na kuwapa mafunzo watangazaji wengine wa kike wa kutangaza habari za taifa.
Anadaiwa kufurahia maisha.
Chun-hee is anadaiwa kutembelea migahawa bora zaidi na vituo vya burudani Pyongyang.
No comments:
Post a Comment