Most Popular

Iran na Tanzania kuimarisha uhusiano wa kiutamaduni

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeazimia kuimarisha uhusiano wa kiutamaduni na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkuu wa ICRO na Waziri wa Utamaduni Tanzania
Hayo yamesema na Mkuu wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu la Iran, (ICRO) Bw. Abudhar Ibrahim Turkman leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wa Tanzania Mhe. Nape Moses Nnauye. Katika kikao hicho Bw. Turkman amesema kuna nukta nyingi za pamoja za kiutamaduni baina ya Iran na Tanzania na jambo hilo limeandaa uwanja wa kuimarisha ushirikiano baina ya nchi mbili. Aidha amesisitiza kuwa, Wairani wameacha athari za kudumu za kiutamaduni nchini Tanzania.

Ibrahimi Turkman ametoa wito wa kutekelezwa makubaliano ya kiutamaduni baina ya Iran na Tanzania sambamba na kufanyika wiki ya utamaduni ya nchi mbili katika miji ya Dar es Salaam, Kilwa, Tehran na Shiraz.

Kwa upande wake, Waziri Nnauye alisema kuwa amekubaliana na wazo la kuanzishwa kwa wiki ya utamaduni kati ya Tanzania na Iran na kwamba ni fursa pekee ya kujifunza kutoka kwa Wairani namna ya kukuza, kulinda na kuuendeleza utamaduni wa Mtanzania
Posted By: MJOMBA ZECODER

Iran na Tanzania kuimarisha uhusiano wa kiutamaduni

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger