Most Popular

Air China yaomba radhi baada ya kushtumiwa ubaguzi

Shirika la ndege la China la Air China limeomba radhi baada ya kutuhumiwa kujihusisha na mambo ya ubaguzi kwa abiria wanaosafiri na ndege zake, na hivyo kulazimika kuondoa gazeti lake lililozua utata katika ndege zake.

Wachina wanaona kwamba usalama wao unapaswa kufuatiliwa katika maeneo yote.
Shirika la Air China lilionya abiria wanaosafiri na ndege zake kuwa waangalifu katika maeneo ya mji wa London ambapo wanaishi "Wahindi, Wapakistan na watu weusi" na kutokwenda nje wakati wa usiku katika mitaa ya mji mkuu wa Uingereza.

Mbunge wa mji wa London, Virendra Sharma mwenye asilia ya India, amemuomba balozi wa China kuomba radhi.

"Ninasikitika na kushangaa kuona leo, baadhi ya watu wanafikiria kuwa inakubalika kuandika vithibitisho ambavyo ni uongo mtupu na ubaguzi wa rangi.

"Mhariri wa gazeti la shirika la ndege la Air China ameomba radhi.

Amehusisha "maelezo yasiyo kuwa na muafaka" kwa makosa ya uhariri.

Lakini kwenye mitandao ya kijamii, Wachina wanaona kwamba maneneo yaliyoandikwa na shirika la ndege la Air China si ya ubaguzi wa rangi au matusi kwa Uingereza.
Wanaona kwamba usalama wao unapaswa kupewa kipaumbele katika maeneo yote duniani.


Posted By: MJOMBA ZECODER

Air China yaomba radhi baada ya kushtumiwa ubaguzi

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger