Most Popular

HABARI KUHUSU JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI




 

Bunge la Uganda kutumia Dola 177,000 kuwatuza wabunge medali

 Kiongozi wa upinzani nchini humo Kizza Besigye na mkewe Winnie Byanyima ni miongoni mwa wabunge wa zamani watakaopata medali hizo.ENDELEA

 

 

Wahisani wajitokeza kuwasaidia waathiriwa wa tetemeko la ardhi nchini Tanzania

Jengo lililoporomoka mjini Bukomba nchini Tanzania baada ya tetemeko la ardhi
 Zaidi ya Shilingi za Tanzania Bilioni 1 zimeahidiwa katika mkutano kati ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na wahisani hao wakiwemo wafanyibiashara waliokutana siku ya Jumanne jijini Dar es salaam.ENDELEA


15.09.2016

Mawasiliano yakwamisha kuanza kwa kesi ya ugaidi nchini Kenya

 Mmoja wa washukiwa hao Shukri Haji, ambaye ni kiziwi ameiambia Mahakama kuwa alikuwa haelewi kile ambacho mtafsiri wa lugha ya ishara alikuwa anamwambia.ENDELEA

10.10.2016
Kenya: Mahakama yawaruhusu wasichana wavae hijab wawapo shuleni
Wasichana wa kiislam wanaosoma shule nchini Kenya wanapaswa kuruhusiwa kuvaa hijab kama sehemu ya sare zao za shule , imeamuru mahakama ya rufaa.ENDELEA


09.09.2016

Viongozi wa EAC wakubaliana kuhusu mkataba wa kibiashara na EU

 Mkataba huu utawezesha bidhaa kutoka mataifa ya EAC kutotozwa ushuru katika soko la Ulaya ilimradi tu ziwe katika hali nzuri.ENDELEA

09.09.2016

Viongozi wa EAC wakubali mapendekezo ya mratibu wa mazungumzo ya Burundi

 Rais Magufulu amesema kuwa, walipokea taarifa ya mratibu wa mazungumzo ya amani ya Burundi, Rais Mkapa, ambaye tayari ameshazikutanisha pande zinazokinzana nchini Burundi katika mazungumzo aliyoyafanya jijini Arusha na Brussels.ENDELEA
07.09.2016

Wakuu wa EAC kukutana Dar es Salaam, Burundi, Sudan Kusini kuwa ajenda

 Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC, wanatarajiwa kukutana mwishoni mwa juma hili jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania, kuanzia September 8 hadi 9, ambapo masuala kadhaa yanatarajiwa kujadilia.ENDELEA


Posted By: MJOMBA ZECODER

HABARI KUHUSU JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger