Wahisani mbalimbali wakiwemo Mabalozi wa nchi za 
kigeni wameahidi kusaidia kujenga upya makaazi na miundo mbinu muhimu 
iliyoharibika kama shule nchini Tanzania baada ya kutokea kwa tetemeko 
la ardhi  mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Bukoba Magharibi mwa nchi 
hiyo.
![]()  | 
| Jengo lililoporomoka mjini Bukomba nchini Tanzania baada ya tetemeko la ardhi | 
Zaidi ya Shilingi za 
Tanzania Bilioni 1 zimeahidiwa katika mkutano kati ya Waziri Mkuu Kassim
 Majaliwa na wahisani hao wakiwemo wafanyibiashara waliokutana siku ya 
Jumanne jijini Dar es salaam.
Tetemeko hilo la ardhi ndio janga baya zaidi kuwahi kuikumba nchi hiyo ya Afrika Mashariki katika siku za hivi karibuni.
Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na tetemeko hilo la ardhi lenye ukubwa wa ritcha 6, imefikia watu 17 huku mamia wakiendelea kupewa matibabu.
Siku ya Jumatatu, rais wa nchi jrani ya Kenya Uhuru Kenyatta, alitangaza kuwa serikali yake inatoa msaada wa mabati, magodoro na vifaa vingine vya ujenzi kuwasaidia waathiriwa tetemeko hilo.

No comments:
Post a Comment