Most Popular

Bunge la Uganda kutumia Dola 177,000 kuwatuza wabunge medali

Bunge nchini Uganda linatarajiwa kutumia Dola za Marekani 177,000 kuwatuza medali wabunge 1,200 waliohudumu katika bunge la nchi hiyo kati ya mwaka 1962 hadi 2012.

Lango la kuingilia Bunge la Uganda jijini Kampala
Vyombo vya Habari nchini humo vinaripoti kuwa sherehe za kuwatuza wabunge hao zitafanyika mwishoni mwa mwezi huu katika maadhimisho ya miaka 50 ya bunge hilo.

Kiongozi wa upinzani nchini humo Kizza Besigye na mkewe Winnie Byanyima ni miongoni mwa wabunge wa zamani watakaopata medali hizo.

Raia wa Uganda, wameonekana wakipinga matumizi ya fedha hizo katika sherehe hizo wakati huu raia wa nchi hiyo wakiendelea kukabiliana na hali ngumu ya kiuchumi.

Hatua hii imekuja baada ya Gazeti la serikali ya New Vision kutangaza kuwa bunge limepanga kutumia fedha hizo kufanikisha shughuli hiyo.

Wabunge 13 wamefariki dunia  kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Posted By: MJOMBA ZECODER

Bunge la Uganda kutumia Dola 177,000 kuwatuza wabunge medali

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger