Mradi unaolenga kupunguza idadi ya
wasichana wanaopata mimba mapema kwa kutumia watoto bandia nchini
Australia, huenda umesababisha matokeo ambayo hayakuwa yanatarajiwa ama
ambayo hayakutakikana.
Lengo lilikuwa kuwazuia kupata mimba ya mapema na kuwafanya kuelewa usumbufu na matatizo ambayo watu hukumbana nayo wakiwalea watoto.
Washiriki wa mpango huo uliotekelezwa magharibi mwa Australia pia walipewa mafunzo ya afya ya uzazi.
![]() |
Add caption |
Uchunguzi uliofanywa baada ya wasichana hao kutimiza miaka 20 ulibaini kwamba asilimia 8 wakati huo walikuwa wamejifungua angalau mara moja na asilimia 9 walikuwa wametoa mimba.
Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa katika jarida la kimatibabu la Lancet.
Watafiti wanasema baadhi ya sababu ambazo huenda zilifanya mradi huo kutofanikiwa ni kwamba haukuangazia wavulana, ambao pia huchangia katika wasichana kushika mimba.
Aidha, huenda watafiti walichelewa kuanza kuwafunza wasichana waliokuwa tayari wamejiunga na shule za upili.
Aidha, wanasema watoto bandia hawawezi wakaonyesha kwa njia halisi taswira ya kumtunza mtoto halisi.
No comments:
Post a Comment