Most Popular

Mbwa achaguliwa tena kuwa meya Minnesota, Marekani

Mbwa mmoja katika jimbo la Minnesota, Marekani amechaguliwa tena kuhudumu kama meya wa mji mmoja katika jimbo hilo.

Mbwa huyo kwa jina Duke ana umri wa miaka tisa na alichaguliwa mara ya kwanza kuwa meya wa mji wa Cormorant mwaka 2014, kwa mujibu wa kituo cha habari cha WDAY kituo ambacho kina ushirikiano na shirika la habari la ABC.

Mpinzani wake katika uchaguzi huo, Richard Sherbrook, alipata kura mbili au tatu.

Wadhifa wa meya wa Cormorant huwa wa staha na watu huhitajika kulipa dola moja ili waruhusiwe kupiga kura.
Duke alichaguliwa mara ya kwanza kuwa meya 2014

Mmiliki wa mbwa huyo David Rick aliambia wanahabari kwamba mara ya kwanza mbwa huyo kuchaguliwa ilikuwa kibahati lakini baadaye ameibukia kupendwa sana na wakazi.

"Kila mmoja alimpigia kura Duke, isipokuwa mtu mmoja aliyempigia kura mpenzi wake Duke, Lassie," Rick aliambia WDAY.

Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2014, watu 12 walishiriki.

Mji huo, ambao kwa mujibu wa ABC News ulianzishwa 1874, kwa sasa una wakazi takriban 1,000.
Kuchaguliwa kwa Duke kuwa meya wa Cormorant miaka miwili iliyopita kulitokea siku chache baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa meya wa mji jirani wa Dorset, Robert Tuff, mvulana wa miaka mitano, baada ya kuhudumu kwa miaka miwili.

"Hakuna mtu angeweza kunikamata, hata maafisa wa polisi," alisema Tuff wakati wa kuondoka kwake, akisema alifurahia sana kipindi chake madarakani.
Alimwachia majukumu Eric Mueller, 16.

Stubbs aliyechaguliwa meya wa mji wa Talkeetna, Alaska.

Duke si mnyama wa kwanza kuchaguliwa kuongoza. Miaka karibu 20 iliyopita, paka kwa jina Stubbs alichaguliwa meya wa mji wa Talkeetna katika jimbo la Alaska.

Mji huo unapatikana kilomita 185 kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo hilo, Anchorage.

Posted By: MJOMBA ZECODER

Mbwa achaguliwa tena kuwa meya Minnesota, Marekani

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger